Monday, 7 November 2016

Dondoo Tatu (03) Zitakazokusaidia Kupata Mada za Kuandika Katika Blogu

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!



Rafiki kati ya maswali yanayoulizwa na waandishi wanaanza kuandika (beginners) ni mada gani waichague kuandika makala katika blogu. Lakini pia kwa wale ambao wameanza kuandika huwa wanajiuliza nijikite katika mada gani katika kuendelea kuandika makala katika blogu.
Katika makala hii napenda kukushirikisha maeneo matatu ambayo tunakutana nayo au tumeshakutana nayo (common) lakini tumekuwa hatuyapi kipaumbele au kuwa na mtazamo wa kupata mada za kuandika katika blogu zetu.

Soma Makala Hii Inayohusiana; Hatua Nne (04) Katika Uandishi wa Blogu

(a) Andika kuhusu mada unayopenda kujifunza.
Kwa mfano ukikuta unapenda kusoma au kununua vitabu vya masuala ya mafanikio, basi fahamu hilo ni eneo mojawapo ambalo unaweza kuandika. Pia ikiwa una mtu ambaye ni mtaalamu wa kada fulani unayependa kumuuliza maswali kwa ajili ya kujifunza , basi fahamu hilo ni eneo lingine pia unaweza kuandika.
Rafiki ukiyaandika haya ambayo unajifunza unakuwa umewasaidia wengine kupata maarifa ambayo umejifunza.
(b) Andika kuhusu mambo unayopenda kufanya
Ukitafakari miaka yako mitano iliyopita, utagundua kuna kitu au vitu fulani umekuwa unapenda kuvifanya. Katika vitu hivi utagundua kuna mambo umekuwa ukiyafanya yakisukumwa na shauku ya wewe kuyafanya.
Rafiki unaweza ukayaona haya mambo ni ya kawaida kwako, lakini kuna watu ambao wanashauku na wanapenda kufanya mambo sawasawa na wewe ulivyoyafanya lakini hawana watu wa kuwasaidia kuwaongoza, ukiyaandika utakuwa umewasaidia kuwa role model wao kupitia yale unayoyaandika.
(c) Andika kuhusu mambo uliyopitia katika maisha yako
Kutokana na sehemu ulizoishi au sehemu ulizofanya kazi kuna uzoefu ambao  umekuwa ukiujenga hatua kwa hatua, siku hadi siku. Uzoefu huu ni hazina kubwa ambao unaweza kuwasaidia wale ambao wanaanza katika maeneo hayo.
Rafiki mambo haya uliyoyapitia katika maisha unaweza kuandika ili kuwasaidia waweze kuepuka makosa ambayo wewe uliyafanya  lakini pia waweze kutumia muda mfupi zaidi kuliko ambao uliuutumia kutokana na kukosa kocha wa kukusaidia.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Related Posts:

  • Fursa nyingi, Muda mchache na Rasilimali chache, Nifanyaje?Ukifanya uchambuzi kwa kulinganisha kundi la "shughuli na fursa" na kundi la "muda na rasimali" utapata hitimisho ya kuona katika kundi la "shughuli na fursa" zipo nyingi kuliko kundi la "muda na rasilimali" tulizonazo kwa aj… Read More
  • Uwekaji Mipango UsioaminikaNi asili yetu kuwa na matumaini mema juu ya jambo fulani ambayo yamepitiliza uhalisia. Mfano tunadhani kuwa tutafanya mambo mengi kwa muda mchache kuliko inavyotakiwa kiuhalisia au kudhani jambo unalolifanya litachukua muda m… Read More
  • Usipobadilika, utamezwa na mabadilikoYanapotokea mabadiliko jifunze kukabiliana nayo (kuadapt) kwa haraka vinginevyo utakavochelewa zaidi kwa kutafakari nini cha kufanya na kulialia na hali halisi utatumia gharama kubwa kuyapokea na muda utakuwa umekwenda pia. … Read More
  • Msingi wa kutimiza maisha yenye ufanisiUwezo uliopo ndani yetu ni mkubwa sana kuliko kile ambacho tumeshakitendea haki kwa nafasi zetu tulizonazo kwa kutendea ulimwengu. Maswali haya yatakusaidia kutafakari kitu gani ambacho unacho ndani yako bado hujakileta ulimw… Read More
  • Maliza Robo ya Kwanza 2015 Hivi Hatua 3 muhimu unazohitaji kuzichukua ili kuweza kutumia muda wako kwa ufanisi na kupata matokeo ya ndoto yako kwa haraka: 1. Have a Plan Kuwa na mpango wa kina unaoanisha nini unachotaka kufanya na mpango huu ni lazima uw… Read More

2 comments:

  1. Asante Mushi kwa ushauri, naomba utembelee www. Umburifodders. Blogspot. Com unipe comment zako. Kazi zako nzuri.

    ReplyDelete
  2. Ludovick Anael,naomba unitumie barua pepe yako kwa ajili ya kukutumia comments. Ahsante
    Tuko pamoja.

    ReplyDelete