Monday, 7 November 2016

Dondoo Tatu (03) Zitakazokusaidia Kupata Mada za Kuandika Katika Blogu

Habari rafiki yangu ambaye ni mfuatiliaji wa makala katika blogu hii ya Stadi za Mafanikio!



Rafiki kati ya maswali yanayoulizwa na waandishi wanaanza kuandika (beginners) ni mada gani waichague kuandika makala katika blogu. Lakini pia kwa wale ambao wameanza kuandika huwa wanajiuliza nijikite katika mada gani katika kuendelea kuandika makala katika blogu.
Katika makala hii napenda kukushirikisha maeneo matatu ambayo tunakutana nayo au tumeshakutana nayo (common) lakini tumekuwa hatuyapi kipaumbele au kuwa na mtazamo wa kupata mada za kuandika katika blogu zetu.

Soma Makala Hii Inayohusiana; Hatua Nne (04) Katika Uandishi wa Blogu

(a) Andika kuhusu mada unayopenda kujifunza.
Kwa mfano ukikuta unapenda kusoma au kununua vitabu vya masuala ya mafanikio, basi fahamu hilo ni eneo mojawapo ambalo unaweza kuandika. Pia ikiwa una mtu ambaye ni mtaalamu wa kada fulani unayependa kumuuliza maswali kwa ajili ya kujifunza , basi fahamu hilo ni eneo lingine pia unaweza kuandika.
Rafiki ukiyaandika haya ambayo unajifunza unakuwa umewasaidia wengine kupata maarifa ambayo umejifunza.
(b) Andika kuhusu mambo unayopenda kufanya
Ukitafakari miaka yako mitano iliyopita, utagundua kuna kitu au vitu fulani umekuwa unapenda kuvifanya. Katika vitu hivi utagundua kuna mambo umekuwa ukiyafanya yakisukumwa na shauku ya wewe kuyafanya.
Rafiki unaweza ukayaona haya mambo ni ya kawaida kwako, lakini kuna watu ambao wanashauku na wanapenda kufanya mambo sawasawa na wewe ulivyoyafanya lakini hawana watu wa kuwasaidia kuwaongoza, ukiyaandika utakuwa umewasaidia kuwa role model wao kupitia yale unayoyaandika.
(c) Andika kuhusu mambo uliyopitia katika maisha yako
Kutokana na sehemu ulizoishi au sehemu ulizofanya kazi kuna uzoefu ambao  umekuwa ukiujenga hatua kwa hatua, siku hadi siku. Uzoefu huu ni hazina kubwa ambao unaweza kuwasaidia wale ambao wanaanza katika maeneo hayo.
Rafiki mambo haya uliyoyapitia katika maisha unaweza kuandika ili kuwasaidia waweze kuepuka makosa ambayo wewe uliyafanya  lakini pia waweze kutumia muda mfupi zaidi kuliko ambao uliuutumia kutokana na kukosa kocha wa kukusaidia.
Rafiki unaweza kuwashirikisha wengine kuhusu blogu hii kwa ajili ya kupata maarifa mbalimbali na pia unaweza kubofya hapa ili kuweza kupata makala kila inapowekwa kupitia barua pepe yako.

Related Posts:

  • Fanya Haya ili Ukue1. Usitamani mambo yangekuwa marahisi, tamani ungekuwa bora mno Don't wish it were easier; wish you were better 2. Usitamani ungekutana au ungekuwa na matatizo machache,tamani ungekuwa na ujuzi zaidi Don't wish for less prob… Read More
  • Sumu ya MafanikioUnapokosa lengo kubwa katika maisha yako kwa kutokujua nini hasa unahitaji na unakipataje, mara nyingi hupelekea kutegemea maoni au ushauri wa watu wengine zaidi katika kuamua kitu cha kufanya kwa ajili ya maisha yako badala … Read More
  • Usipuuze TatizoMatatizo mengi kamwe hayatatuliwi au hayadhibiti kwa ufanisi kutokana na kutoyapa uzito wa kutosheleza. Hakuna tatizo ambalo halina umuhimu kiasi kuwa hatuhitaji kujali kuhusu hilo tatizo. Mfano kwa mwanafunzi inawezekena hap… Read More
  • Tazama Kushindwa kwa Jicho HiliKushindwa hakuamaanishi wewe ndiye uliyeshindwa bali kunamaanisha hujafanikiwa bado Kushindwa hakumaanishi haukutimiza/haujafanikisha kitu bali kunamaanisha umejifunza kitu Kushindwa hakumaanishi wewe ni mjinga bali kunamaa… Read More
  • Je, Unajua?Ni bora kufanya kitu kisicho kamili kuliko kutokufanya chochote kisicho na dosari Better to do something imperfectly than to do nothing flawlessly… Read More

2 comments:

  1. Asante Mushi kwa ushauri, naomba utembelee www. Umburifodders. Blogspot. Com unipe comment zako. Kazi zako nzuri.

    ReplyDelete
  2. Ludovick Anael,naomba unitumie barua pepe yako kwa ajili ya kukutumia comments. Ahsante
    Tuko pamoja.

    ReplyDelete